The House of Favourite Newspapers
gunners X

Watu 10 Wafariki, 18 Wajeruhiwa kwa Ajali mikese Morogoro

0

Watu 10 wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha magari mawili kugongana uso kwa uso, katika eneo la maseyu kata ya mikese barabara kuu ya Morogoro – Dar es salaam

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Morogro Alex Mkama amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo na imehusisha basi aina ya Mitsubish Fuso mali ya Kampuni ya Mawio lenye namba za usajili T 162 DMD, likitokea Morogoro kuelekea Mombo, mkoani Tanga na lori lenye namba za usajili T 956 ELU lenye tela namba T 828 ELW

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari la mizigo kuhamia upande wa kulia zaidi alipokuwa akiyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari

hali ya mvua kubwa inayoendelea kunyesha na kusababisha kugongana uso kwa uso kisha magari yote kuwaka moto na kuteketea. Uchunguzi zaidi unaendelea ikihusisha utambuzi wa miili ya marehemu.

Leave A Reply