Watu 13 Wafariki Dunia na Wengine Kujeruhiwa Baada ya Moto Kuteketeza Klabu ya Usiku
Watu 13 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia moto mkubwa kulipuka na kuiteketeza klabu moja ya usiku katika Mji wa Murcia, Kusini Mashariki mwa Hispania.
Mamlaka nchini humo zimeeleza kuwa moto huo ulizuka majira ya alfajiri ya kuamkia leo, katika klabu maarufu ya Teatre ambapo bado chanzo cha moto huo hakijajulikana.
Kipande cha video kilichowekwa na jeshi la zimamoto nchini humo, kinawaonesha maafisa wa zimamoto na uokoaji wakipambana na moto huo ambapo inaelezwa kuwa huenda idadi ya vifo ikaongezeka.
Mamlaka ya Mji wa Murcia imetangaza siku tatu za maombolezo ambapo bendera zote zitapepea nusu mlingoti.