160 Wafariki Kwa Maporomoko ya Barafu
IDADI ya watu waliofariki kutokana na maporomoko ya barafu kaskazini mwa Pakistan, imefikia zaidi ya 100 huku wengine 94 wakijeruhiwa na makazi kuharibiwa.
Mpaka sasa nyumba nyingi bado zimefunikwa na vifusi vya barafu huku shughuli za uokozi zikiendelea huko Kashimir, lakini watu wengi zaidi wanahofiwa kufariki kutokana na kufunikwa na vifusi hivyo.

Waziri Mkuu wa Pakistan, Raja Farooq Haider Khan, ameyaagiza mashirika yanayoshughulikia majanga ya kitaifa nchini humo kwenda eneo hilo kuwasaidia waathirika wa janga hilo.
Vilevile, jeshi la nchi hiyo linaongoza shughuli za uokozi kwa kutumia helikopta zao na vifaa vingine.

