The House of Favourite Newspapers

Watu 18 Wauawa katika Mashambulizi Dhidi ya Msikiti wa Afghanistan

0
Waliouawa

TAKRIBANI watu 18 wameuawa na wengine 23 kujeruhiwa katika mashambulizi yaliyotokea katika msikiti mmoja mkubwa huko Herat Magharibi mwa Afghanistan.

 

Tukio hilo limetokea Septemba 2, 2022 baada ya mlipuko mkubwa kutokea eneo hilo ikiwa ni siku chache tangu Imamu mashuhuri wa msikiti huo, Mujib ur Rahman Ansari kutangaza kwamba iwapo mtu yeyote atapinga utawala wa Talibani atapaswa kukatwa kichwa.

Imamu mashuhuri wa Msikiti wa Gazaghah, Mujib ur Rahman Ansari ambaye ni miongoni mwa watu waliouawa msikitini hapo

Imamu Mujib aliyasema hayo Julai, mwaka huu wakati akizungumza katika mkutano wa viongozi wa dini uliofanyika katika Mji wa Kabul nchini humo.

 

Msemaji wa serikali ya nchi hiyo, Zabihullah Mujahid amesema kuwa Imamu Ansar ambaye ni mfuasi mkuu wa Taliban ameuawa kikatili katika shambulio hilo.

Shambulio

Mujahid ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter na kueleza kuwa amesikitishwa na kifo chake huku akitoa ahadi kwa watu wote waliohusika katika tukio hilo wataadhibiwa vikali kutokana na vitendo vyao viovu.

 

Picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha miili iliyotapakaa kwenye jengo la msikiti wa Gazaghah na vyombo vya habari vya nchi hiyo vimeripoti kuwa vinahofia kuwepo kwa majeruhi wengi.

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave A Reply