The House of Favourite Newspapers

Watu 19 Wafariki Baada ya Kutokea Shambulio la Kujitoa Muhanga

0
Watu 19 wameuawa katika shambulio hilo

TAKRIBANI watu 19 wamefariki baada ya kutokea shambulio la kujitoa muhanga kwenye Chuo Kikuu kilichopo katika Mji wa Kabul nchini Afghanistan.

 

Taarifa hiyo imetolewa na Polisi wa Mji wa Kabul na kueleza kuwa licha ya shambuli hilo kuua watu lakini pia limejeruhi watu kadhaa.

 

Maafisa kutoka chuo hicho wamesema kuwa elimu inayotolewa katika eneo la Dasht-e-Barchi Magharibi mwa Mji wa Kabul ni ya ziada na shambulio lilitokea wakati ambao wanafunzi wakifanya mitihani.

Majeruhi wa tukio hilo

Aidha, wameongeza kuwa wahanga wengi wa tukio hilo ni wale wanaoishi katika eneo hilo ambao wanatoka katika kabila la Hazara ethnic lenye watu wachache zaidi.

 

Picha za eneo hilo zilizosamba kwenye televisheni na mitandao ya kijamii zilionesha matukio kutoka karibu na hospitali, ambako mstari wa miili ya watu iliyofunikwa ilikuwa imelazwa chini sakafuni.

Wanafunzi wakijisomea kabla ya tukio kutokea

Vyombo vya habari vya nchi hiyo viliripoti uharibifu uliotokea ambapo vilionekana vifusi vya majengo, madawati ya shule kuharibika na madaraja yaliyoboka.

 

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave A Reply