The House of Favourite Newspapers

Watu 20 wauawa katika mapigano Bangui

0

Vijana wakiziba barabara kwa kuchoma matairi.

Daktari mmoja wa jeshi ameiambia shirika la habari la AFP kuwa zaidi ya watu 100 walijeruhiwa katika makabiliano baina ya waislamu na wakristu katika eneo la PK-5.

Wenyeji wa Bangui wakitoroka makwao kufuatia ghasia hizo.

Makabiliano hayo yalitibuka baada ya mauaji ya mwendesha bodaboda ambaye alikuwa ni muislamu.
Eneo hilo la PK-5 ndilo lililokuwa chimbuko la mapaigano ya wenyewe kwa wenye kati ya waislamu na wakristu kati ya mwaka wa 2013- 2014.Maafisa wa kijeshi wa umoja wa mataifa walioko huko walilazimika kuingilia kati ili kukomesha maafa zaidi.

Serikali ya mpito imekashifu mauaji hayo iliyoyataja kuwa ya kipuuzi.Taifa hilo limekuwa likijaribu kurejea katika uongozi wa kiraia na wa amani kufuatia vita vilivyotokea baada ya kundi la waasi wa Seleka ambao wengi wao ni Waislamu walipoipindua serikali ya Francois Bozize inayoungwa mkono na makundi ya wakristu ya “anti-balaka”.

Kwa sasa makundi ya wakristu “anti-balaka” yanadhaniwa kushiriki katika mapigano hayo ya kulipiza kisasi na kuna hofu kubwa kuwa huenda kukaibuka mapigano zaidi.

Leave A Reply