The House of Favourite Newspapers

Watu 30 wauawa msikitini Nigeria

0

MSIKITI

(Picha na Maktaba)

TAKRIBANI watu 30 wamepoteza maisha nchini Nigeria baada ya mabomu mawili kulipuliwa katika msikiti mmoja uliopo jimbo la kaskazini mashariki la Borno.

Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema, shambulio hilo lilifanyika wakati wa swala ya Magharibi jana jioni baada ya watu wawili kujilipua kwa mabomu ndani ya msikiti huo.

Mukhtar Ahmadu, mfanyabiashara karibu na msikiti huo amesema watu wote waliokuwa wakitekeleza ibada ya Swala ya Magharibi wameuawa katika shambulio hilo.

Ameongeza kuwa Waislamu wengi walikuwa ndani ya msikiti huo kutekeleza ibada ya swala.

Mpaka sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na hujuma hiyo lakini vyombo vya serikali ya Nigeria vinalinyooshea kidole cha tuhuma kundi la kigaidi la Boko Haram.

Shambuluzi hilo limefanyika siku mbili tu baada ya milipuko kadhaa ya mabomu iliyoua watu wasiopungua saba huko Maiduguri.

Credit: kiswahili.irib.ir

Leave A Reply