Watu 36 Wamefariki Dunia na Wengine Zaida ya 50 Kujeruhiwa Katika Ajali ya Train India.
Mashuhuda wakiangalia Treni iliyopinduka.
INDIA: Katika jimbo la Andhra Pradesh huko India watu 36 wamefariki dunia na wengine wengi zaidi ya 50 kujeruhiwa baada ya Treni ya abiria kuacha reli na kupinduka. Maafisa wamethibisha taarifa hizo.
Ramani ikionesha eneo ilipotokea ajari, (Andhra Pradesh)
Idadi ya vifo inaongezeka kutokana na majeruhi wengi kuumia vibaya hivyo idadi ya vifo inaendelea kuongezeka kulingana na muda unavyokwenda.
Bado haijafahamika wazi chanzo cha ajari hiyo lakini maafisa bado wanaendelea na uchunguzi.
Mr Mishra mmoja kati ya maafisa waokoaji alisema majeruhi wamepelekwa hospitali mbili zilizopo jirani na eneo la tukio .
Comments are closed.