Watu 37 Wafariki kwa Shambulio la Mgodi

SHAMBULIO la kushtukiza lililolenga msafara wa wafanyakazi wa mgodi wa Canada nchini Burkina Faso, limesababisha vifo vya watu 37, hili likiwa shambulio baya zaidi kuwahi kutekelezwa katika kipindi cha miaka 5.

Shambulio hili ni mfululizo wa mashambulizi yanayotekelezwa na makundi ya wanajihadi yanayoendelea kutatiza usalama kwenye nchi za ukanda wa Sahel.

 

Polisi nchini humo imesema watu waliokuwa na bunduki walishambulia msafara wa mabasi 5 yaliyokuwa yamewabeba wafanyakazi wa ndani na mainjinia wanaofanya kazi na mgodi wa Samafo.

Tukio hili limejiri wakati huu Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Florence Parly akiwa ziarani kwenye mataifa ya ukanda wa Sahel ambapo ametangaza kuanza kwa operesheni za kijeshi dhidi ya makundi ya wanajihadi.


Loading...

Toa comment