The House of Favourite Newspapers

Watu 64 Wanaswa na Muroto, Wamo Wezi, Makahaba na Wauza Madawa – Video

Jeshi la Polisi linaendelea na misako katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma ambapo limefanikiwa kukamata mali za wizi, wapokeaji wa mali za wizi na wezi wa kuvunja nyumba za watu jijini humo.

 

Akizungumza na wanahabari jijini humo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Girres Muroto amesema katika msako unaoendelea wamekamatwa watuhumiwa 64 wa makosa mbalimbali na mali mbalimbali za wizi.

 

Amesema wamemkamatwa MSAFIRI STEPHANO (32), Mgogo na mkazi wa CHAMWINO akiwa na mafuta aina ya Diesel kiasi cha dumu 5 za lita 20 sawa na lita 100 zinazodhaniwa kuwa ni mali ya wizi kinyume cha sheria.

 

Ameongeza kuwa, wahalifu wa aina hii ni hatari kwani wanahujumu maendeleo ya Taifa kwa kuhujumu miradi mbalimbali.

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma litawakamata wahalifu wote wanaohujumu miradi ya maendeleo ya taifa. Uchunguzi wa kina unafanyika ili kubaini watuhumiwa wengine na watafikishwa mahakamani.

 

Mbali na halo, Muroto amesema Jeshi hilo limefanikiwa kuwanasa akina dada 11 wanaodaiwa kuwa ni makahaba na wengine waliyokamatwa na madawa ya kulevya aina ya bangi ambapo wote wanaendelea kuhojiwa.

VIDEO: MSIKIE MUROTO AKIFUNGUKA

Comments are closed.