The House of Favourite Newspapers

Watu 7 Wafariki Dunia Baada ya Kula Nyama ya Kasa Anayedhaniwa Kuwa na Sumu

0

Watu saba wakazi wa Mafia mkoani Pwani, wamefariki dunia baada ya kula samaki aina ya kasa anayedhaniwa kuwa na sumu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Canute Msacky amesema mnamo Machi 12, 2023 majira ya saa moja za usiku katika Kijiji cha Bweni na Kijiji cha Kanga, Kata ya Kanga Tarafa ya Kaskazini, Wilaya ya Mafia mkoa wa kipolisi Rufiji, watu saba 7 kutoka kaya nne tofauti walibainika kufa baada ya kula nyama ya samaki aina ya kasa anayesadikiwa kuwa na sumu.

Waliofariki katika tukio hilo ni Abdalah Hatibu Nyikombo (4), Mshirazi mkazi wa Bweni, Makame Hatibu Nyikombo (9), mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Bweni na Mohamed Juma Makame (miezi 7), Mshirazi mkazi wa Bweni.

Wengine ni Ally Selemani (miezi 8), Mndengereko mkazi wa Kanga, Salima Mjohi (28), mshirazi mkulima mkazi wa Bweni, Minza Juma Hatibu (miezi 10) mndengereko mkazi wa Bweni na Ramadahani Karim (miezi 8), Mndengereko, mkazi wa Bweni.

Miili ya marehemu hao imefanyiwa uchunguzi wa kitabibu katika Hospitali ya Wilaya ya Mafia na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Leave A Reply