Watu 9 wafariki baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutumbukia mtoni Kenya
WATU tisa wamethibitishwa kufariki baada ya basi walimokuwa wakisafiria kutumbukia kwenye mto Mbagathi uliopo jijini Nairobi, vimeripoti vyombo vya habari nchini nchini humo.
Basi hilo mali ya Naboka Sacco lilikuwa likielekea Nairobi kutoka Gataka, katika mtaa maarufu wa Karen wakati dereva ambaye ni miongoni mwa waliopoteza maisha, aliposhindwa kulimudu gari na kuacha Barabara.
Watu sita walifariki papo hapo huku wengine wawili wakifariki walipokuwa wakipatiwa matibabu.
Polisi wamesema kuwa dereva alikosa udhibiti wakati breki ya gari ilipokatika.