Watu 90 Wafariki kwa Mafuriko

TAKRIBAN watu tisini wamefariki na wengine karibu  400,000 kuachwa bila makao kufuatia mafuriko makubwa Sudan.

 

Umoja wa Mataifa unasema mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini humo tangu mwisho wa mwezi Julai.

 

Viwango vya maji katika ziwa vimepanda hadi karibu mita 17.5,  kiwango ambacho ni cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 100.

 

Maeneo yaliyoathirika vibaya ni mji mkuu wa Khartoum, Sudan Mashariki, White Nile na Darfur ambako maelfu ya watu sasa wanahitaji msaada wa dharura.

 

Baadhi ya watu walioathiriwa na mafuriko hayo ni wale ambao walikuwa wametoroka makwao kutokana na mzozo na tayari walikuwa wamepoteza njia za kujipatia kipato kufuatia janga la corona.

 

Umoja wa Mataifa unasema ukosefu wa maji safi wakati huu wa janga la virusi vya corona unawaweka katika hatari ya kupata maambukizi.

Toa comment