The House of Favourite Newspapers

Watu 92 Wauawa Katika Maandamano Nchini Iran, Mashirika ya Haki za Binadamu Yabainisha

0
Rais wa Iraq, Ibrahim Raisi

TAKRIBANI watu 92 wameuawa kwa madai ya ukandamizaji unaofanywa nchini Iran wa kutuliza maandamano yaliyochochewa na kifo cha mwanamke anayefahamika kwa jina la Mahsa Amini.

 

Shirika la Haki za Binaadamu la Iran (IHR) lenye makao yake katika Mji wa Oslo na Amnesty International lenye makao yake mjini London, yamesema zaidi ya watu 41 walifariki dunia katika ghasia zilizotokea Septemba 30, 2022.

Ghasia zilizosababisha vifo vya watu 92

Maandamano hayo yamefanywa na wanawake wa Iran ambao wamekuwa wakichoma moto hijabu walizokuwa wakilazimika kuzivaa tangu mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979.

 

Wakati maandamano hayo yakifikia wiki ya tatu, Rais wa Iran, Ebrahim Raisi amesema kwamba maadui wa Iran wameshindwa na njama zao.

Maandamano

Mkurugenzi wa Shirika la Haki za Binaadamu la Iran, Mahmood Amiry-Moghaddam ameitaka jumuia ya kimataifa kuchukua hatua za haraka dhidi ya serikali ya Iran na kukomesha mauaji ya waandamanaji huku akieleza kwamba huo ni sawa na uhalifu dhidi ya binadamu.

 

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave A Reply