The House of Favourite Newspapers

Watu na tuzo zao England, Acha Kabisa!

Manchester United's Swedish striker Zlatan Ibrahimovic (L) celebrates with Manchester United's French midfielder Paul Pogba after scoring their second goal from the penalty spot during the English Premier League football match between Manchester United and Southampton at Old Trafford in Manchester, north west England, on August 19, 2016. / AFP / Oli SCARFF / RESTRICTED TO EDITORIAL USE. No use with unauthorized audio, video, data, fixture lists, club/league logos or 'live' services. Online in-match use limited to 75 images, no video emulation. No use in betting, games or single club/league/player publications.  /         (Photo credit should read OLI SCARFF/AFP/Getty Images)London, England

TUZO ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu England imekuwa maarufu sana kwa siku za hivi karibuni.

Tuzo hiyo imeanza muda mrefu na imekuwa ikitolewa na wachezaji wengi sana ambao wamekuwa wakionyesha kiwango cha juu kwa mwezi husika.

roomeyStaa wa Manchester United, Wayne Rooney ni kati ya wachezaji ambao wamekuwa na rekodi ya kuitwaa mara nyingi akiwa ameshaitwaa mara sita tu tangu ilipoanzishwa. Msimu huu umekuwa bora sana kwa baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa wakionyesha kiwango cha juu.

Kuna wale ambao awali walitarajiwa kuwa wakitua England wanaweza kuitwaa tuzo hiyo kila msimu akiwemo kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Paul Pogba, lakini ajabu mambo kwao ni magumu. Chini ni wachezaji waliotwaa tuzo hiyo tangu msimu huu umeanza, Agosti mwaka jana

AGOSTI:

raheem-sterlingRaheem Sterling

AGOSTI:

Kwa sasa unaweza kuwa humsikii sana, lakini ukweli ni kwamba Raheem Sterling alianza msimu huu kwa kasi na kufanikiwa kuwa mchezaji bora wa Agosti. Huu ulikuwa mwezi wa kwanza tu tangu msimu ulipoanza na timu yake ya Manchester City ilianza vizuri sana.

Hii ilikuwa tuzo ya kwanza ya mchezaji huyo kwenye Ligi Kuu England na aliipata baada ya kufunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao ndani ya mwezi huo. Winga huyo aliwashinda Eden Hazard wa Chelsea, Antonio Valencia (Manchester United) na Curtis Davies (Hull City). Hata hivyo, kuanzia hapo timu hiyo haikuweza kufanya vizuri na kwa sasa ipo katika nafasi ya tano kwenye Ligi Kuu England.

heung-min-sonSEPTEMBA:

Staa wa Tottenham, HeungMin Son alifanya maajabu kwa mwezi Septemba na kufanikiwa kuwashinda vigogo na kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi huo. Kiungo huyo alikuwa na mwezi bora sana baada ya kuwashinda mastaa, Kevin De Bruyne wa Manchester City, Theo Walcott (Arsenal) na Adam Lallana (Liverpool), N’Golo Kante na Diego Costa (wote wa Chelsea).

victor-mosesNOVEMBA:

Huu hadi sasa ni msimu wa Chelsea baada ya mchezaji wa timu hiyo Victor Moses kufanikiwa kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Novemba. Hii ni timu pekee ambayo wachezaji wake wawili hadi sasa wameshatwaa tuzo hiyo baada ya Eden Hazard kuitwaa mwezi Oktoba.

Moses ambaye hakuwa ameonyesha kiwango cha juu msimu uliopita ameamka tena na sasa ni moto wa kuotea mbali. Moses, 25, alifanikiwa kuiongoza timu hiyo kushinda michezo yote mitatu ya ligi hiyo kwa mwezi Novemba ambayo ni dhidi ya Everton, Middlesbrough na Tottenham Hotspur.

Mchezaji huyo raia wa Nigeria anakuwa wa kwanza kutoka Afrika kutwaa tuzo hiyo msimu huu. Alifanikiwa kuwashinda Gylfi  Sigurdsson wa Swansea, Nordin Amrabat (Watford), Victor Anichebe (Sunderland), Sergio Aguero (Manchester City) na Matt Phillips (West Brom).

skysports-man-united-premier-league-zlatan-ibrahimovic_3825374DESEMBA:

Mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amekuwa mchezaji bora wa ligi hiyo kwa mwezi Desemba akiwashinda wachezaji kadhaa mahiri.  Zlatan amefanikiwa kuwashinda Alexis Sanchez, Diego Costa na Dele Alli wa Totenham na kufanikiwa kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya kwanza tangu alipotua England mwanzoni mwa msimu huu.

Ibrahimovic, 35, alifanikiwa kufunga mabao matano kwenye michezo sita ya mwezi Desemba na kuiongoza timu yake kucheza mwezi mzima bila kufungwa.

Hadi sasa Ibrahimovic amefanikiwa kufunga mabao  19 kwenye michezo 28 ya Ligi Kuu England.

during the UEFA EURO 2016 Qualifier match between Italy and Bulgaria on September 6, 2015 in Palermo, Italy.

MAKOCHA BORA WA MWEZI:

Pamoja na kwamba kumekuwa na wachezaji bora wa mwezi, tuzo hiyo imekuwa ikiambatana na ile ya makocha bora wa mwezi. Kuanzia mwezi Agosti hadi kufi kia sasa kuna makocha watatu ambao wameshatwaa tuzo hiyo kutokana na kuzisimamia timu zao kufanya vizuri.

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte ameweka rekodi ya kuwa kocha pekee ambaye ameshatwaa tuzo hiyo mara tatu kwa msimu mmoja, wengine ni: Mike Phelan, Hull City (Agosti) Jürgen Klopp, Liverpool (Septemba) Antonio Conte, Chelsea (Oktoba) Antonio Conte, Chelsea (Novemba) Antonio Conte, Chelsea (Desemba).

MAKOCHA WANAOONGOZA KUTWAA TUZO HIYO

A. Ferguson  27

A. Wenger  15

D.Moyes  10

M.O’Neill   8

MABAO BORA MSIMU HUU:

Pia kila mwezi limekuwa likitangazwa bao bora la mwezi kwa wachezaji wote wanaoshiriki kwenye ligi hiyo, hadi sasa kuna wachezaji wanne ambao wameshatwaa tuzo hiyo. Bao la mwisho lilifungwa na Henrikh Mkhitaryan mwezi Desemba ambalo lilizua gumzo sana:

MWEZI          JINA                TIMU

Agosti:          S. Mane           Liverpool

Septemba:   J.Henderson Liverpool

Oktoba:       G. Ramirez     Middlesbrough

Novemba:   P.Rodríguez     Spurs

Desemba:  H. Mkhitaryan Man. UTD

Comments are closed.