The House of Favourite Newspapers

Watu saba wafariki kwa ajali ya helikopta, New Zealand

0

Helikopta (2)Mabaki ya helikopta hiyo baada ya ajali.Helikopta (3)…Ikiwa angani kabla ya ajaliHelikopta (1)Eneo la ajali.
Helikopta (4)
Helikopta (5) Milima na mabonde kwenye eneo la Fox GlacierHelikopta (6)

Barafu zikiwa zimetanda.

New Zealand

WATU saba wakiwemo watalii wa Kiingereza wanne, raia wa Australia wawili pamoja na rubani wamefariki kwenye ajali ya helikopta mapema leo nchini New Zealand.

Ajali hiyo imetokea baada ya helikopta hiyo yenye injini moja wakati ikipaa angani, kuanguka kwenye bonde lililo na barafu katika huko South Island eneo la Fox Glacier lililopo kwenye ufukwe wa Magharibi mwa nchi ya New Zealand.

Picha zilizopatikana zinaonesha helikopta hiyo ikiwa imenasa katikati ya miamba miwili mikubwa kwenye bonde hilo.

Mpaka sasa helikopta nne zimetumwa eneo hilo kutafuta mabaki ya ndege na kutoa miili ya marehemu licha ya changamoto zilizopo eneo hilo ikiwa ni pamoja na miamba mingi, barafu na milima na mabonde hivyo kufanya vikosi vya uokoaji kushindwa kufika kwenye eneo la tukio kirahisi

Ajali kama hiyo ilitokea mwaka 2010 wakati ndege iliyokuwa imebeba waruka mwavuli ilipoanguka baada ya kupaa angani kutoka Fox Glacier na kuua watu tisa.

Leave A Reply