The House of Favourite Newspapers

Watu watatu wamefikishwa mahakama ya London kwa kusaidia ujasusi

0

Watu wote kutoka kusini mashariki mwa Uingereza walikamatwa mwezi huu na kushtakiwa kwa uingiliaji wa kigeni

Watu watatu walifikishwa katika mahakama ya London Jumatatu baada ya kushtakiwa kwa kuisaidia idara ya ujasusi ya Hong Kong. Chung Biu Yuen mwenye miaka 63, Peter Wai mwenye miaka 38, na Matthew Trickett mwenye miaka 37, waliachiliwa kwa dhamana baada ya kesi kusikilizwa kwa muda mfupi katika Mahakama ya Westminster.

Washukiwa hao watatu, wote kutoka kusini mashariki mwa Uingereza walikamatwa mapema mwezi huu na kushtakiwa kwa uingiliaji wa kigeni na kuisaidia idara ya ujasusi ya kigeni, walikiuka sheria ya usalama wa taifa ya Uingereza, polisi walisema Jumatatu.

Sheria hiyo ya usalama ambayo ilipitishwa mwaka jana, inaruhusu polisi kuwakamata washukiwa katika kesi za usalama wa taifa na uhaini bila kibali. Serikali ya Uingereza imesema sheria hiyo inalinda taifa dhidi ya “tishio la vitendo vya uhasama kutoka kwa mataifa yanayolenga demokrasia, uchumi na maadili ya Uingereza”.

Leave A Reply