The House of Favourite Newspapers

WATUHUMIWA 22 BIASHARA YA UKAHABA MIKONONI MWA MUROTO – VIDEO

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watuhumiwa 29 wakiwemo makahaba 22 waliokuwa wakifanya bishara ya ngono, wanaume watano waliokuwa wakinunua pamoja na wamiliki wanne wa maeneo yanayoruhusu biashara hizo.
Hayo yamesemwa leo Jumanne, Oktoba 9, 2018 na Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto, wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema  kati ya watuhumiwa hao wanawake ni 22 na wanaume wa tano pia limewakamata wamiliki wanne wa maeneo yanayodaiwa kuruhusu kufanyika kwa ukahaba.
“Katika Operesheni hiyo wahalifu wanaofanya makosa ya udhalilisha wa utu dhidi ya Maadili  tumewakamata  watuhumiwa 29, Makahaba 22, wanaume watano watano na wamiliki  wanne wa maeneo ambayo yanaruhusu kufanyika kwa biashara ya ukahaba ,” amesema Muroto.
Kamanda Muroto amesisitiza kuwa biashara hiyo haitakiwi katika Jiji hili kwani kuna kazi nyingi za kufanya ili kujipatia kupata na si kuuza miili yao ambayo ni kinyume cha sheria ya kanuni ya adhabu sura 16 kifungu cha 146 hivyo watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

VIDEO: FUATILIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.