The House of Favourite Newspapers

Watumiaji Wa Mitandao Wamshambulia Raisi Wa Burundi

 

Watumiaji wa mtandao wa Twitter wameunga mkono hatua ya wasichana watatu wa shule kwa kuzichora na kuharibu picha za rais wa Burundi Pierre Nkurunziza wakiiga mfano wao.

 

Picha zilizoharibiwa za kiongozi huyo zinasambazwa katika mitandao ya kijamii chini ya alama ya reli ya #FreeOurGirls. Wasichana hao walishtakiwa wiki iliopita wakimtusi kiongozi huyo wa taifa na wanaweza kuhudumia kifungo cha miaka mitano jela.

 

Mamlaka nchini Burundi hushtumiwa kwa kukabiliana na haki za kibinaadamu na wale wanaopinga serikali. Wasichana hao walio na kati ya umri wa miaka 15, 16 na 17 walikamatwa wiki mbili zilizopita baada ya picha za rais huyo kuchorwa katika vitabu vya kusoma .

 

Wanafunzi wengine wanne waliokuwa wamekamatwa pamoja nao waliachiliwa baadaye. Hizi hapa baadhi ya picha ambazo zimekuwa zikisambazwa mtandaoni zikiwaunga mkono wasichana hao.

 

Baba ya mmoja ya wasichana hao aliambia kundi moja la kampeni Human Rights Watch kwamba walikuwa waoga kula.

 

HRW wameagiza serikali kuwaachilia wasichana hao na kuendelea kukabiliana na matusi yanayofanywa na vikosi hivyo vya usalama.

 

Mamlaka inafaa kuwakamata wale waliotekeleza ukiukaji mkubwa wa haki za kibinaadamu badala ya kuwafunga jela wasichana kwa kuchora picha ya rais alisema Lewis Mudge.

 

Katika kisa kama hicho 2016, wasichana kadhaa walifungwa jela na mamia kufukuzwa shuleni kwa kuzichora picha za rais.

Comments are closed.