The House of Favourite Newspapers

Watumiaji wa Yas Waukaribisha Mwaka Mpya kwa Furaha ya Mamilioni

Mkurugenzi wa Masoko wa Yas, Edwardina Mgendi, (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi mshindi wa shilingi milioni tano, Agnes Njau. Kushoto ni Msemaji wa Kampeni ya Magift ya Kugift, Haji Manara.

Dar es Salaam, 3 Januari 2025: Kampuni ya mtandao wa simu ya Yas, kupitia kampeni yake ya Magift ya Kugift, leo wamendelea kukabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wa kampeni hiyo kwenye droo ya 8, akiwemo mshindi wa shilingi milioni tano, Bi. Agnes Michael Njau na kuwafanya waukaribishe mwaka mpya kwa furaha ya mamilioni hayo.

Miongoni mwa washindi hao ni wale waliojishindia kiasi cha shilingi milioni moja kila mmoja pamoja na wa milioni tano Bi Agnes Njau ambapo mshindi wa gari jipya na la kisasa aina ya Kia Seltos 0.km naye anatarajiwa kukabidhiwa gari lake muda wowote kuanzia sasa.

Mkurugenzi wa Masoko wa Yas, Edwardina Mgendi, (kushoto) na Msemaji wa Kampeni ya Magift ya Kugift, Haji Manara (kulia) wakiwa na washindi washindi.  

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi zawadi hizo kwa washindi, Mkurugenzi wa Masoko wa Yas, Edwardina Mgendi, amesema anayofuraha kuona wanakabidhi zawadi kwa washindi wa droo hiyo ya nane 8.

Edwardina ameendelea kusema kuwa huo ni utaratibu wao kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu na zawadi nyinginezo kwa wateja wao katika kipindi hiki cha kuelekea siku kuu za mwisho wa mwaka.

Mgendi  amesema mpaka sasa wameshatoa zawadi za fedha zenye thamani ya  kiasi cha  TSh milion 244, kwa washindi wa makundi  tofauti ikiwemo, mawakala na wateja wengine na kuwataka wengine kutumia huduma za Yas ili waweze kuibuka na ushindi kwenye droo zilizobaki.

Kwa upande wao, washindi wa wiki hii, Agnes Michael Njau na Said Rashid Athumani wakiwakilisha wenzao ambao wamejinyakulia kiasi cha Shilingi milioni moja wameishukuru kampuni ya Yas kwa kuendesha kampeni ya Magift ya Kugift na hatimaye kuwazawadia zawadi hizo. Amesema Agnes.

Hii ni wiki ya nane kati ya wiki 12 ambazo Yas imeendelea kuwagiftisha wateja wake kwa kutumia huduma mbalimbali za kampuni hiyo ikiwemo muda wa maongezi, kununua salio kwa Mixx by Yas, kufanya malipo mbalimbali na kutuma pesa kwenda mitandao mingine kwa kutumia Mixx by Yas.