Watumiaji wa Yas Wazidi Kunufaishwa na Magift ya Kugift
Dar es Salaam 17 Januari 2025: Kampuni ya mtandao wa mawasiliano ya Yas Tanzania, imekabidhi zawadi kwa washindi wa Promosheni ya ‘Magift Kugift’ droo ya 10.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo kwa washindi wa wiki hii Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Yas, Mwangaza Matotola amesema wanayofuraha kuwapatia washindi hao wa wiki hii na pia amewaomba Watanzania kuendelea kutumia huduma za Yas ikiwa ni pamoja na kufanya miamala.
Kampuni ya Yas Tanzania imekuwa ikiendesha kampeni hii wiki ya 12 sasa ambapo zaidi ya kiasi cha Shilingi zaidi ya mil. 300 za Kitanzania zimeshatolewa zikienda kwa washindi mbalimbali sambamba na zawadi nyinginezo ikiwemo simu za mkononi.
Kwa upande wake mmoja wa washindi wa milioni moja 1 wa wiki hii Patrick Daniel Manimba, ameishukuru Yas kwa kuja na kampeni hiyo na kusema imekuwa ikiwapatia zawadi kubwa za pesa na vitu vingine wateja wake ambazo wamekuwa hawakuzitegemea hivyo kubadili au kuwasogeza kimaisha.
Naye mshindi wa milioni tano wiki hii, Husna Ali Mwinyi amesema yeye ameibuka mshindi na hatimaye kipigiwa simu baada ya kufanya miamala mara kwa mara jambo lililopelekea kuibuka mshindi hivyo amewataka wananchi wengine kutumia mtandao wa Yas kwani ni mtandao wenye huduma bora na unaowajali wateja wake. Alisema Husna.