The House of Favourite Newspapers

Watumiwa Wa Ubakaji Wafikishwa Mahakamani Dodoma

0

WATUHUMIWA wanne waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kubaka na kulawiti na baadae picha mjongeo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua hakaruki wamefikishwa mahakamani leo Agosti 19, 2024 jijini Dodoma.

Watuhumiwa hao wamefikishwa katika kituo jumuishi cha utoaji haki, Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma na kusomewa makosa mawili ambapo kosa la kwanza nia Kubaka kwa kundi na kosa la pili ni kumuingilia kinyume cha maumbile binti huyo.

Watuhumiwa hao waliofikishwa mahakamani ni MT. 140105 Clinton Honest Damas maarufu Nyundo,Amin Lord Lema, Nickson Idala Jackson na C.1693 Playgod Edwin Mushi

Kwa mujibu wa taarifa ya Renatus Mkude, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka amesema kesi hiyo itasikilizwa kwa siku tano kuanzia leo Agosti 19 hadi Agosti 23 siku ya Ijumaa.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania mkoani Dodoma, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Mashtaka Makao Makuu, Renatus Mkude amesema vijana hao wamekana mashtaka hayo na kutokana na unyeti wa shauri hilo wataendelea kuwa mahabusu.

Leave A Reply