Wauzaji Wa Magazeti Wang’ara Global
ILIKUWA ni shangwe ndani ya Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori jijini Dar jana baada ya wauzaji wa magazeti 16 kupewa vyeti kutokana na mchango wao wa kuwa na kampuni kwa zaidi ya miaka 10.
Wauzaji hao waliokabidhiwa zawadi zao ni wale wanaotokea jiji la Dar ambao wametoa mchango wao kwa kampuni kwa muda wote huo hadi sasa.
Akizungumza katika mkutano huo, muuza magazeti Mohamed Juma Mbunge alisema kuwa, imekuwa jambo kubwa kwani hakuna kampuni iliyowahi kutoa zawadi kama hiyo.
“Nitoe shukrani zangu kubwa kwa Eric Shigongo (Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group) kwa heshima aliyotupa, tangu nimekuwa muuza magazeti sijawahi kuona kampuni ikifanya kitu kikubwa kama hiki, tunashukuru sana,” alisema Mbunge.
Muuzaji mwingine, Juma Ikhala alipongeza kampuni ya Global kuja na gazeti namba moja la michezo la Spoti Xtra linalotoka kila Jumapili kupunguzwa bei kutoka shilingi 800 hadi 500 na pia kuliongezea siku na kuwepo siku ya Alhamisi.
“Nashauri hili Spoti Xtra litoke hata Jumanne tena litakuwa vizuri kwani limeshiba na linastahili, nawapongeza Global kwa hii zawadi,” alisema Ikhala.
Comments are closed.