The House of Favourite Newspapers

Wauzaji Mbogamboga Soko Kuu Kariakoo Wajigamba na Betika

MAPEMA leo Jumatano Novemba 13, 2019, timu ya maofisa masoko ya Global Publishershers imetembelea maeneo ya Soko Kuu la Kariakoo ambapo wauzaji wa mbogamboga hufanyia biashara zao na kujipatia gazeti la Betika ambapo wengi wao walionesha kufurahia kuletewa eneo la biashara zao ambapo pia walitambua mchango wa gazeti hilo hususani kwenye masuala ya kubeti.

Betika ambalo hutolewa bure kwa wenye umri kuanzia miaka 18, linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers na huingia mtaani kila Jumatano.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara.

Baadhi ya wasomaji waliokutana na timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, walizidi kulisifia gazeti hilo kuwa gumzo kila kona ya nchi na kurahisisha kwenye masuala ya michezo ya kubeti.

 

Gazeti hilo heshima yake imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia Betika kwa bei nafuu.

Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

Comments are closed.