Wawa Apewa Mwaka Mmoja Simba

BEKI wa kati wa Simba raia ya Ivory Coast, Pascal Wawa, ameandaliwa mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia timu hiyo.

 

Wawa ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, ameandaliwa mkataba mpya baada ya timu hiyo kuachana na Junior Lokosa Junior.

 

Mtu wa karibu na mchezaji huyo, ameliambia Championi Jumatano kuwa: “Kwa sasa Simba wana mpango wa kumuongeza Wawa mkataba wa mwaka mmoja baada ya Junior Lokosa kuondoka na mkataba huo atasaini hivi karibuni.

 

“Simba wanavutiwa na Wawa ambaye amekuwa na pacha nzuri na Onyango (Pascal) ambaye amejiunga na timu hiyo msimu huu pia ukiangalia tangu atue amekuwa kikosi cha kwanza mara kwa mara.

 

Alipotafutwa Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu simu yake iliita bila kupokelewa.

STORI: CAREEN OSCAR, Dar es Salaam

Toa comment