The House of Favourite Newspapers

Wawa Awashangaa Wanaobeza Kiwango Chake

BEKI wa kati wa Simba, Pascal Wawa amewashangaa wanaodai uwezo wake umefikia mwisho na wala hana hofu kama Simba itaamua kumtema kwani bado anaamini kiwango chake kipo juu.

Beki huyo ambaye licha ya kutambulishwa na uongozi wa timu hiyo lakini inaelezwa hajasaini mkataba wowote kwa kuwa alipewa nafasi ya kujaribiwa katika mi­chuano ya Kombe la Kagame iliyomalizika hivi karibuni.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Wawa alisema kuwa kwa upande wake hana wasiwasi wowote iwapo Simba itaamua kumua­cha kufuatia madai ya kutokuwa na kiwango kama inavyodaiwa na baadhi ya mashabiki.

“Kiukweli hilo jambo limenishtua, akina nani wanasema nimeisha uwezo wa kucheza mpira na kwa nini, hao hawajui wanachokisema hawajui chochote mimi bado nipo sawa na uwezo wangu haujashuka wala nini.

 

“Sina cha kuhofia najua wapi nimetoka na uwezo wangu upoje hata uon­gozi ukiamua kuniacha sina hofu ni sawa tu kwa sababu Mungu ndiyo anajua kila kitu na siku zote nimekuwa nikimua­mini yeye tu.

 Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

Comments are closed.