Kartra

Wawa: Yanga Msijisahau, Bado Tunajambo Letu

BEKI wa kati wa Simba, Pascal Wawa raia wa Ivory Coast ameibuka na kutoa kauli ya vitisho kwa wapinzani wao, Yanga katika Ligi Kuu Bara kuwa wasisahau kwa kudhani kuwa Simba haina mpango na ubingwa kutokana na ushiriki wao katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Wawa ametoa kauli hiyo ikiwa Yanga leo Jumamosi inatarajiwa kucheza na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopangwa kupigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa wakati Simba jana usiku ikiwa inacheza na Al Ahly katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na Championi Jumamosi,Wawa alisema kuwa kitendo cha wao kuwa bize na michuano ya kimataifa isiwe sababu ya wapinzani kuona urahisi kwa kuweza kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwa kuwa hata wao bado wana malengo ya msingi.

 

“Unajua hii michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika imekuwa ni migumu sana lakini kadiri tunavyopiga hatua ndiyo matarajio na malengo yetu yanazidi kuwa makubwa maana tumefikia kwenda kucheza robo fainali lakini malengo tufike nusu fainali.

 

“Nadhani kuwa bize huku kusiwe sababu ya wengine kuchukulia kuwa ni sehemu ya kuweza kusahau kuwa bado kuna mechi za ligi kwa sababu licha ya kushiriki Ligi ya Mabingwa bado tunahitaji kushinda ubingwa wa ndani wa ligi hivyo haiwezi kuwa jambo rahisi,” alisema Wawa

STORI: IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam


Toa comment