Vijana Wawili wa Miaka 14 Mbaroni kwa Ubakaji

POLISI mkoani Shinyanga inawashikilia vijana wawili, Boazi Shija (14)na Jakaya John (14), kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye miaka sita (jina limehifadhiwa).Watuhumiwa hao ni wakazi wa Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.

 

Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga, ACP Debora Magiligimba, amesema  vijana hao walimlaghai mtoto huyo kwa pipi na kumpa hela kisha kumpeleka kichakani karibu na eneo analoishi na wazazi wake kisha  kumfanyia unyama huo.

 

Polisi imesema  watawafikisha mahakamani watuhumiwa hao  baada ya upelelezi kukamilika.

Toa comment