The House of Favourite Newspapers

Wawili wafariki, 36 wajeruhiwa katika ajali Morogoro

0

bm1

Basi la BM lenye namba za usajili T619 BOX baada ya kugongana na lori leo eneo la Lubungo Mikese, barabara ya Morogoro-Dar es Salaam.

WATU wawili wamefariki dunia na wengine 36 kujeruhiwa, kati yao wanne vibaya baàda ya basi walilokuwa wakisafiria kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea Morogoro, mali ya kampuni ya BM kuligonga ubavuni lori lililokuwa likija mbele yake na kuangukia kwenye bonde pembeni ya barabara na kupinduka mara nne, katika eneo la Lubungo Mikese, barabara kuu ya Morogoro-Dar es Salaam.

20160123021252Muonekano wa nyuma wa basi hilo.

ITV imefika katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro na kushudia majeruhi wa basi hilo la kampuni ya BM wakiletwa kwa magari binafsi na basi jingine la kampuni hiyo, wakionekana kujeruhiwa zaidi maeneo ya kichwani, usoni na miguuni, ambapo mwandishi alilazimika kuweka kalamu pembeni na kusaidiana na wananchi wengine kuwabeba majeruhi na kuwaingiza kwa madaktari kupata huduma ya kwanza,huku vitanda vya kuwabebea vikionekana kuwa vichache ikilinganishwa na wingi wa majeruhi.  Baadhi ya mashuhuda waliohojiwa wameeleza namna ajali hiyo ilivyotokea na kulalamikia wizi uliofanywa na waliofika eneo la tukio baada ya ajali.

Daktari bingwa wa upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro, Francis Semwene, amekiri kupokea miili ya wanaume wawili na majeruhi 36, ambapo wanne kati yao hali zao ni mbaya na wengine italazimika kuwakata baadhi ya viungo iwapo watashindikana kushonwa.

Leave A Reply