The House of Favourite Newspapers

Wazambia Wanapigwa Tena Kwao

0

RED Arrows wana kazi kubwa zaidi leo ya kufanya mbele ya Simba ndani ya dakika 90 za pili wakiwa nyumbani kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya mtoano.


Wazambia hao wanahitaji
kushinda mabao 4-0 ili kuvuka kwenda hatua ya makundi ya michuano hiyo jambo ambalo Kocha wa Simba, Pablo Franco na viongozi wa timu hiyo wanasema haliwezi kutokea.

Kumbuka mchezo wa kwanza uliochezwa Dar, Simba ilishinda 3-0.Mratibu wa Simba, Abasi Ally, aliliambia Spoti Xtra kuwa mipango yote ya ndani na nje ya uwanja tayari imeshakamilika, kilichobaki ni kwa upande wa wachezaji kutimiza majukumu yao ndani ya dakika 90.


“Mimi kama mratibu
wa Simba nimeshamaliza majukumu yangu ya kuweka mambo sawa ili timu iweze kushinda. Siwezi kusema Red Arrows hawawezi kutufunga 4-0, ila naona wao tukiwafunga mengi zaidi,” alisema.


Kwa upande wa Pablo
alisema kuwa imani yake inamuonesha kuwa vijana wake wanakwenda kushinda tena mchezo huo, kutoka na ubora waliounesha kwenye michezo mitatu ya mwisho na maandalizi aliyofanya juu ya mechi hiyo.


“Natumaini tutasonga
mbele, tutavuka kwa kupata ushindi mzuri tukiwa ugenini, tuna mtaji wa mabao matatu jambo ambalo linatuongezea kujiamini na kufanya vema zaidi,” alisema Pablo.

 

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo Jumapili majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki kwenye Uwanja wa Heroes uliopo Lusaka, Zambia. Mshindi wa jumla atakwenda hatua ya makundi ya michuano hiyo.

STORI NA ISSA LIPONDA, DAR | SPOTI XTRA

Leave A Reply