The House of Favourite Newspapers

Wazazi wa Wanafunzi 55 Kukamatwa Baada ya Watoto Wao Kupewa Ujauzito

Serikali kupitia Mkuu wa Wilaya wa Tandahimba imegiza kukamatwa kwa wazazi wa wanafunzi 55 waliopata ujauzito na kuacha Shule miaka miwili iliyopita.

 

Agizo hilo ambalo limetolewa na  Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambae pia na Mkuu wa wilaya hiyo Sebastian Warioba amesema wazazi wa wanafunzi wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. ili iwe fundisho kwa watu wengine wilayani hapo kutokana na kuongezeka kwa mimba za wanafunzi.

 

Tatizo la mimba kwa wanafunzi katika wilaya ya Tandahimba, Mkoani Mtwara limedaiwa kuongezeka katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Disemba mwaka huu idadi ambayo imepanda kutoka 27 mwaka jana hadi mimba 53.

 

Wakizungumza katika kikao cha Ushauri cha Wilaya DCC, wadau wa kikao hicho wamesema suala la mimba ni changamoto kwa wanafunzi wa shule za sekondari wilayani Tandahimba.

 

Hata hivyo Wajumbe wa kikao hicho wametupa lawama zao kwa vyombo vinavyohusika na ufuatiliaji wa makosa hayo ya kuwapa ujauzito wanafunzi na kusema wanashindwa kuwajibika na kufuata sheria.

Comments are closed.