Wazee wa CCM Arusha Waridhishwa na Maendeleo Tanga
Ikiwa ni mara ya Kwanza kwa Wazee wa Mkoa wa Tanga na Arusha kufanikiwa kuketi meza moja, Mwenyekiti CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdarahman Abdallah amesema, lengo lililopo ni kuhakikisha mikoa hiyo inatwaa viti vyote na hivyo kushika nafasi ya kwanza Chaguzi wa Serikali za mitaa.
Wazee wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoani Arusha wametia nanga katika Jijini la Tanga kukutana na wenzao wa Mkoani humo Mwenyeji wao akiwa Mwenyekiti wa Chama hicho tawala Mkoani Tanga Rajabu Abdarahman Abdallah ambaye pia ni Mlezi wa CCM Arusha.
Katika mazungumzo yake ikiwa ni muda mfupi baada ya kuwapokea Wazee hao wa Arusha, Rajabu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM alisema, lengo la Viongozi hao kukutana ni kutengeneza utaratibu utakaowawezesha kwenda pamoja kuelekea Uchaguzi wa Serikali za kitaa.
“Sisi Tanga tumejipambanua kuhakikisha…uchaguzi wa Serikali za mitaa kushinda viti vyote na kushika namba moja na hata Arusha nilipochaguliwa mlezi wote tutashika nafasi hiyo kwenye uchaguzi wa mitaa na Rais ,Wabunge na madiwani “alisema Rajabu Abdarahman.
Mwenyekiti huyo Mkoa alitumia fursa hiyo kuwaeleza Wazee hao wa kutoka Arusha kuwa Tanga inajivunia ushirikiano ndani ya Chama tawala na hata Serikali kwa ngazi zote ingawa changamoto ndogo ndogo haziwezi kukosekana.
Aidha amepongeza ushirikiano mzuri ambao Chama tawala imekuwa ikiupata kwa Serikali ya Mkoa huo kupitia kwa Mkuu wa Mkoa Balozi Dkt Batilda Burian akimueleza kuwa mtu mchapakazi, mnyenyekevu na pia amekuwa muungwana.
Rajabu Abdarahman Abdallah amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akisema ameweza kuimarisha huduma jamii elimu, fya, maji na hata miundombinu ya Umeme.
Amesema kwamba kwenye Mkoa wa Tanga wenye Vijiji 79 vyote vimewekwa nishati ya umeme na kwamba kimoja kilichosalia tayari transformation imewekwa ili huduma kukamilisha ambapo Serikali itakuwa haina deni.
Kwa upande wa sekta ya afya, Rajabu Abdarahman Abdallah alisema, hapo awali Tanga ilikosa huduma muhimu kama vile CT Scan na ile ya kusafisha figo jambo ambalo liliwalazimu wananchi kufuata huduma hiyo KCMC na Muhimbili lakini sasa yote hayo yanapatikana hospitali ya rufaa ya Bombo.
“Ni Wajibu wetu kama watanzania tuyazungumze mema aliyofanya Rais wetu na Chama chetu wazee wanaweza kuwa mabalozia kueleza yaliyofanywa na Rais,shida ya Wapinzani wamejaaliwa sana uongo”alisema Rajabu.
Kwa upande wake mwakilishi wa Wazee kutoka Mkoani Arusha katika salamu zake alimwelezea Rajabu Abdarahman Abdallah kwamba Kiongozi wa aina yake anayepaswa kupatiwa ushirikiano ili kuendelea kukijenga chama tawala.
Alisema,nyota ya Kiongozi huyo ilianza kung’ara tangu akiwa wilayani Pangani ambapo kwa kiasi kikubwa alifanikiwa kuiunganisha Chama tawala na hata wanachama wake.
“Huyu bwana ni Kiongozi wa kipekee hata hili sikuwa naamini maana haijawahi kutokea kuunganisba wazee tena wa mikoa miwili….ni mtu mwenye busara,hekima na anajua Uongozi Tanga mmepata chombo”alisema.
Wazee hao kutoka watakuwa Mkoani Tanga kwa siku kadhaa kwa lengo la kuzungumza na wenzao wa Chama cha Mapinduzi CCM ikiwa moja ya mbinu za kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa majukumu yao ambao wameelezea kuridhishwa kwao na jinsi mkoa wa Tanga unavyopiga hatua huku kukiwa na fursa lukuki za maendeleo.