Wazee wa Chadema Wampongeza JPM, Wamuomba Hiki… – Video

Baraza la Wazee (CHADEMA), kupitia kwa Mwenyekiti wake, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Hashim Juma Issa limeweka wazi kuwa Tume huru ya uchaguzi inahitajika kwenye chaguzi zijazo.

 

Hashim Issa ameyasema hayo leo  Julai 5, 2019, mbele ya wanahabari ambapo ameeleza kuwa uwepo wa tume huru utasaidia kuwa na uchaguzi huru na wa haki.

 

”Kupitia tume huru raia watakuwa na haki ya kuchagua mtu wanayempenda au chama wanachotaka kiwaongozelakini sio kwa tume hii”, ameeleza.

 

Kwa upande mwingine Mwenyekiti huyo amempongeza Rais Magufuli kwa kuweka utaratibu wa kukutana na makundi mbalimbali, ikiwemo wafanya biashara huku akitumia nafasi hiyo kumuomba apange mkutano na viongozi wa vyama vya siasa.

 

”Tunampongeza kwa kukutana wafanyabiashara na viongozi wa dini kwani ndiyo inatakiwa kufanyika, bado tu kukutana na viongozi wa vyama vya siasa ili tuongee naye”, ameongeza.

 

Wazee wa CHADEMA watuma maombi kwa Rais Magufuli

Loading...

Toa comment