Amesema viongozi wa hao wa dini pamoja na Wananchi kila mmoja kwa nafasi yake walikuwa ni wa kipekee na dua zao zimeweza kusaidia na kwa sasa amerejea kutoa shukrani na kupokea dua zao hizo kwani kwa sasa ameanza kufanya kazi.
“Kwa sasa nimeanza kurudi kwenye majukumu yangu kama kawaida. Kwa hivyo nikaona kabla ya kuanza kuonekana nikiruka huku na kule kwenye majukumu ya kiwizara, nikasema hapana nirudi kwanza nyumbani nipate dua za wazazi wangu, dua za wazee na viongozi wa dini.
Kwa tukio lile kwa sisi tunaoamini, ni mkono wa Mungu ulikuwa mahala pale” amesema Dkt. Kigwangalla.
Aidha, Dkt. Kigwangalla amewatoa hofu wananchi wa jimbo lake juu ya watu waliokuwa wakipitapita jimboni kwa lengo la kulinyemelea na kutoa maneno ya kumkatisha tamaa.
“Kwa waliokuwa wanatembea na wakikesha usiku kucha wakisubiri nife wameanguka. Mungu amesimama mbele yangu, mimi ni mzima naendelea kutekeleza majukumu yangu mdogomdogo mpaka nitakapokuwa imara kabisa. Sasa naanza upya” amesema Dkt. Kigwangalla.
Pia amewahakikishia wananchi hao kuwa kazi za maendeleo ya jimbo hilo zinaendelea na wasaidizi wake wa ofisi ya Mbunge inaendelea kuratibu kwa ukaribu kabisa na milango ipo wazi.
Katika hatua nyingine Wazee wa Mila na Watemi wakiongoza na Chifu Ng’wana Ng’washi wa Wasukuma walifanya tambiko la kichifu la kumtambikia ili akawe tayari kwa kazi za kulitumikia Taifa katika majukumu ya Kibunge na Uwaziri.
Comments are closed.