The House of Favourite Newspapers

Waziri Ammwagia Sifa Rayvanny

0

BAADA ya staa wa Bongo Fleva anayetumikia Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ kuachia wimbo unaotahadharisha juu ya janga lililoikumba dunia la Virusi vya Corona, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamiii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndungulile, amemmwagia sifa kama zote.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Rayvanny alisema kuwa, Serikali imeona umuhimu wa kazi yake hiyo na kuisifia kupitia kwa Waziri Ndugulile ametamka wazi kuwa amefanya kazi nzuri ya kuhamasisha jamii.

 

Alisema kuwa, kwa upande wake si jambo dogo kwani kuna wasanii wengi hivyo wimbo wake kusifiwa na kiongozi kama huyo ni kitu kikubwa ambacho hakiwezi hata kuelezeka.

 

“Siyo kama nimefurahia sana au kujisifia baada ya Serikali yangu kutambua mchango wangu, bali inatia moyo kuona kwamba mtu unafanya kitu kwa ajili ya jamii na pia kitu hicho kupokelewa vizuri, kwangu inanifunza kuwa linapotokea janga la kitaifa au kidunia siyo lazima mtu ulipwe, lakini ishu hapa ni kuifunza jamii kupitia muziki,” alisema Rayvanny ambaye anatamba na Wimbo Corona ambao ni kwa ajili ya kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga na Virusi vya Corona.

 

Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, wimbo huo ulikuwa umetazamwa mara zaidi ya milioni 1.2 kwenye Mtandao wa YouTube.

STORI: KHADIJA BAKARI NA HAPPYNESS MASUNGA, DAR

Leave A Reply