Waziri Aweso Awatunuku Shahada Mbalimbali Wahitimu Chuo Cha Maji
Aweso amesema mageuzi makubwa yamefanyika ili kukifanya chuo hicho kuwa bora zaidi, ikiwamo miundombinu ya majengo na matokeo mazuri yanaonekana.
Waziri Aweso ameainisha kuwa Tanzania imeongoza kwa miaka miwili mfululizo kati ya nchi 40 katika ujenzi wa miradi ya maji na kutambuliwa na Benki ya Dunia.
Ameelekeza wahitimu wa Chuo cha Maji kutumika katika usimamizi na uendelevu wa miradi ya maji nchini na kwamba ili Taifa liendelee linahitaji nguvu kazi.