The House of Favourite Newspapers

Waziri Azindua Mpango wa Waajiri Kutoa Mafunzo kwa Vijana

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waajiri Nchini (ATE), Aggrey Mlimiki, akizungumza.
Naibu Waziriri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde, akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa ATE, Almasi Maige, akiuelezea mpango huo.
Baadhi ya wageni waalikwa katika uzinduzi huo.
Wageni mbalimbali wakifutalilia kilichokuwa kikiendelea.

NAIBU Waziriri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde, amezindua mpango mkakati wa kutoa mafunzo kwa vijana wanaotarajiwa kufanya kazi wakiwa bado vyuoni na wengine wanapokuwa bado hawajaanza ajira.
Mpango huo umezinduliwa leo jijini Dar es Salaam ukiwa umeandaliwa na Chama cha Waajiri nchini (ATE) lengo lake likiwa ni kutoa mafunzo kwa vijana watarajiwa kuelekea katika ajira ili wanapokuwa wameajiriwa wawe wamepata mafunzo na ujuzi wa kile wanachoenda kukifanya.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa ATEi, Almasi Maige, alisema uzinduzi huo ni pamoja na kuwakutanisha waajiri ili kuzungumza nao juu ya namna wanavyoweza kutoa mafunzo kwa vijana kabla ya kuajiriwa.
Alisema waajiri wataweza kuwasaidia vijana walio vyuoni na ambao hawako vyuoni wawe na uwezo wa kufanya kazi kabla ya kuanza rasmi ili kuondokana na usumbufu unaojitokeza kwa baadhi ya vijana wanaotoka vyuoni na kuajiriwa pasipokuwa na uwezo wa kufanya kazi.
Naye Waziri Mavunde aliupongeza mpango huo wa ATE kukutana na waajiri ili kuzungumzia namna wanavyoweza kuwasaidia vijana wanaotoka vyuoni kwa ajili ya kuanza kazi.

 

Na Denis Mtima/GPL

Leave A Reply