The House of Favourite Newspapers

Waziri Dkt. Dorothy Gwajima Atembelea Benki ya Nmb, Ateta na Uongozi

0
Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna (kulia) akiambatana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima 

 

Benki ya NMB imepata nafasi ya kutembelewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima katika ofisi zao za Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna aliembatana na Afisa Mkuu wa Fedha NMB, Juma Kimori, amempokea Mhe. Gwajima na kumuelezea kuhusu masuluhisho yanayogusa moja kwa moja makundi mbalimbali katika jamii.

Lakini pia, aliahidi kushirikiana na serikali kuhakikisha masuluhisho yao yanakuwa chachu ya maendeleo kwa makundi yote katika jamii kwa kuendelea kuwekeza kwenye teknolojia na ubunifu.

Katika salamu zake, Mhe. Gwajima alimpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo pamoja na uongozi mzima wa Benki ya NMB kwa mafanikio waliyoyapata, na kuahidi kuwa balozi mzuri kufikisha fursa zinazotolewa na benki hiyo kwa wananchi ili waweze kujijenga kiuchumi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna (kushoto) akifuatiwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima wakiwa katika picha ya pamoja. 
Leave A Reply