The House of Favourite Newspapers

Waziri Jaffo Atangaza Kuanza kwa Uchaguzi Mdogo – Video

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jaffo,  ametangaza Novemba 24 mwaka huu kuwa ndiyo siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

 

Ameyasema hayo leo, Agosti 23 Jijini Dodoma wakati akitoa maagizo kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa na viongozi mbalimbali kuelekea uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

 

Uchaguzi huo utafanyika ndani ya siku 90 baada ya tangazo kutolewa ambapo kwa viongozi wa vijiji, vitongoji na mitaa nafasi zao zitakoma siku saba kabla ya kuchukua fomu ya kugombea.

 

Zoezi la kupiga kura litaanza saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni na kampeni zitafanyika kwa siku saba kabla ya siku ya uchaguzi, na kila chama kitakachoshiriki uchaguzi kitawasilisha ratiba yake ya kampeni, si chini ya siku saba kabla ya kuanza kwa kampeni.

“Ofisi ya mkoa ndiyo itakuwa mratibu mkuu wa uchaguzi wa serikali za mitaa katika mkoa husika, ambapo halmashauri za wilaya zitawajibika kuratibu uchaguzi kwa mujibu wa maelekezo yaliyoonyeshwa katika mwongozo,” amesema na kuongeza:

 

“Kwa mujibu wa kanuni hizi, viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita, ukomo wa uongozi wao utakuwa ni siku saba kabla ya siku ya kuchukua fomu kuanza.”

Comments are closed.