The House of Favourite Newspapers

Waziri Kairuki Ashiriki Baraza Tendaji La Shirika La Utalii Duniani

0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki (Kulia) akiwa katika Mkutano wa 121 wa Baraza Tendaji la Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani ( UNWTO).

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeshiriki ufunguzi wa Mkutano wa 121 wa Baraza Tendaji la Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani ( UNWTO) unaofanyika leo Juni 11,2024 jijini Barcelona, Hispania huku ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki (Mb).

Waziri wa Utalii na Viwanda wa Hispania, Jordi Hereu

Akifungua mkutano huo, Waziri wa Utalii na Viwanda wa Hispania, Jordi Hereu amesema kuwa Shirika la Utalii Duniani linaongeza kasi ili kukamilisha utekelezaji wa Mkakati Endelevu wa Utalii wa mwaka 2030 ambao unalenga kuweka mfumo wa kimataifa wa kutokomeza umaskini uliokithiri, kupambana na ukosefu wa usawa na ukosefu wa haki, na kurekebisha mabadiliko ya hali ya hewa hadi 2030.

Tanzania ni mwanachama kamili wa Shirika la Utalii Duniani na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Shirika hilo kwa kipindi cha miaka minne (2023 – 2027).

 

Leave A Reply