The House of Favourite Newspapers

Waziri Kigahe Azindua Upanuzi Mkubwa wa Kiwanda cha Bia cha SBL Mjini Moshi

0
Waziri Kigahe (kulia) akizindua kiwanda hicho.

 

Moshi, Novemba 22, 2022: Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) wameshiriki katika uzinduzi wa upanuzi wa kiwanda cha bia cha Serengeti, tawi la Moshi leo Jumanne Novemba 22, 2022 mjini Moshi.

 

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe, aliyehudhuria tukio hiyo akiwa Mgeni Rasmi, alisema upanuzi wa kiwanda hiko ni tukio kubwa kwa sababu inaonyesha kiwango cha uwekezaji SBL inaendelea kufanya nchini ili kuongeza tija, na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa kutoa fursa za ajira ,na kwa wakulima wa ndani kupata soko la mazao yao.

Kabla uzinduzi msafara wa waziri pamoja na viongozi wa kiwanda hicho wakikagua mitambo ya kisasa iliyofungwa kwenye kiwanda hicho.

 

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi, Naibu Waziri aliipongeza SBL kwa mitambo na vifaa vya kisasa vinavyoendeshwa kwa teknolojia ya kisasa.

 

“Serikali imefurahishwa sana na uwekezaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti katika sekta ya viwanda. Tena tunatambua kuwa uwekezaji huu umekuja katika kipindi ambacho Serikali yetu inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inajitahidi kupunguza urasimu katika uwekezajina kutoa motisha kubwa kwa wawekezaji kuja Tanzania, kwa sababu ndiyo nchi sahihi yenye sera za kuvutia na fursa mbali mbali za uwekezaji.

Waziri Kigahe (katikati) akiangalia mazingira ya kiwanda hicho.

 

Watu wetu wanapata fursa za ajira na wakulima wanaweza kupata soko la mazao yao ikiwa makampuni mengi kama SBL yataendelea kuwekeza,” alisema.

 

“Kampuni ya SBL imetoa mchango mkubwa katika uchumi wa nchi kwa kutengeneza ajira nyingi na kulipa kodi zinazosaidia bajeti ya nchi yetu tena, mchango wake katika kuwainua wakulima kwa kununua mazao yao ni wa mfano wa kuigwa na ushiriki wake katika shughuli mbalimbali za kijamii hapa nchini ni wa kupongezwa wakati wote.” Aliongeza.

 

Upanuzi wa kiwanda cha bia cha Serengeti mjini Moshi ni sehemu ya uwekezaji wa miaka mitatu wa SBL katika kupanua biashara hiyo ambayo imegharimu takriban shilingi bilioni 185 katika matumizi ya mtaji.

 

Kati ya mwaka 2019 na 2020, shilingi bilioni 31 ziliwekezwa katika kiwanda cha bia cha Dar es Salaam Shilingi bilioni 13.4 katika ujenzi wa kituo cha uzalishaji wa vinywaji vikali na shilingi bilioni 124 katika upanuzi wa kiwanda cha kuzalisha bia mjini Moshi, uliofaofanyika kati ya mwaka 2021 na 2022.

 

Mwaka jana, kampuni ya bia ya Serengeti ilitumia shilingi bilioni 15.7 nyingine kupanua kiwanda chake cha bia cha Mwanza. Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Mark Ocitti akizungumzia uwekezaji huo alisema, “kiwango hiki cha uwekezaji hakika ni kielelezo tosha cha imani tuliyonayo sisi Serengeti Breweries na Diageo, mbia wetu mkuu, katika uongozi wa Serikali ya Tanzaniakuunda mazingira dhabiti ambayo biashara zinaweza kustawi.

 

“Aliendelea kwa kusema kwamba kwa kujitolea katika kiwango hiki cha uwekezaji, SBL haiwi tu kama mshirika wa kutegemewa wa uwekezaji katika safari ya kiuchumi ambayo sote tunaianza, lakini pia kama balozi anayestahili wa nchi kwa wawekezaji wengine ambao, kama sisi, watatafuta fursa za uwekezaji.

 

Zaidi ya nusu ya chapa za bia za SBL hutengenezwa kwa asilimia 100 ya malighafi za kienyeji (kama mahindi, shayiri na mtama), ambazo hutolewa kutoka kwa mtandao wa wakulima kote nchini ambao wanapokea usaidizi wa kiufundi na kifedha kutoka kwa kampuni katika shughuli zao za kilimo. Wakulima hawa kwa pamoja huipatia SBL zaidi ya tani 20,000 za nafaka kwa mwaka, zikichukua zaidi ya 80% ya mahitaji yetu ya malighafi.

 

SBL hutengeneza aina mbalimbali za vileo, zikiwemo bia na vinywaji vikali.Bia kuu ni pamoja na Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Guinness Stout, Guinness Smooth na Pilsner Lager.Bidhaa hizi zote zimepokea tuzo nyingi za ubora ndani ya nchi na kimataifa.

SBL ilikamilisha kituo cha kisasa cha uzalishaji wa vinywaji vikali mwaka jana, kilichoruhusu kampuni kuanza kuzalisha pombe kali nchini.

 

KUHUSU SBL:

 

SBL iliyoanzishwa mwaka 1988 kama Associated Breweries, ni kampuni ya bia ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania, na chapa zake za bia zimechukua nafasi ya zaidi ya 25% ya soko kwa ujazo.

 

SBL ina mitambo mitatu ya uendeshaji Dar es Salaam, Mwanza na Moshi. Tangu kuanzishwa kwa SBL mwaka wa 2002, biashara hiyo imekuza jalada lake la chapa mwaka hadi mwaka.

 

Upatikanaji wa hisa nyingi na EABL/Diageo mwaka 2010 umeongeza uwekezaji katika viwango vya ubora wa kimataifa na kusababisha nafasi kubwa za kazi kwa wananchi wa Tanzania.

Leave A Reply