The House of Favourite Newspapers

Waziri Kikwete Alivyozindua Tamasha la Kuwachangia Wenye Changamoto ya Afya ya Akili

0
Waziri Kikwete akikagua moja ya timu zilizoshiriki tamasha hilo nyuma yake mwenye fulana nyeupe ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Exim Bank, Jaffari Matundu.

Dar es Salaam, 29 Septemba 2024: Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete amezindua  Tamasha la  Exim Bima Festival ambalo lengo ni kurudisha kwa jamii ambapo imeshafanya hivyo na kuchangia kiasi cha shilingi milioni mia tatu kwa muda wa miaka mitano ili kurudisha kwa jamiii na kiasi hicho safari hii kitapelekwa kwa wagonjwa wenye changamoto ya afya ya akili.

Akizungumza na wanahabari kwenye Viwanja vya Ghymkhan jijini lilipofanyika tamasha hilo, Waziri Kikwete amesema kuwa fedha zinazopatikana zinakwenda  kuchangia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwenye wenzetu wenye tatizo la afya ya akili.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Exim Bank, Jaffari Matundu akizungumza na wanahabari kwenye tamasha hilo.

Tumekuja kusapoti na kuunga mkono sisi kama Serikali tuko pamoja nao kuhakikisha kwamba jambo hili linafanikiwa.

Kwa upande Afisa Mtendaji Mkuu wa Exim Bank, Jaffari Matundu amesema wao kwao utamaduni wa kurejesha kwa jamii wanachokipata ni wa kamawida na wamesha fanya mambo mbalimbali kama kuchangia damu, kuchangia madawati kwa shule mbalimbali.

Hivyo kwa mwaka huu wao na makampuni mengine ya bima wameona waje na Tamasha la Exim Bima kwaajili ya kuwachangia watu wenye afya ya akili kwa kuwa changamoto hiyo kwasasa imeonekana kuwa kubwa hivyo wao watahakikisha wanaendelea kusaidia ili kupunguza tatizo hilo au kulimaliza kabisa. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA NEEMA ADRIAN/GPL

Leave A Reply