Waziri Kitila Mkumbo Atembelea Kiwanda cha Vioo Mkoani Pwani
Prof. Kitila Mkumbo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji leo Agosti 9, 2023 amefanya ziara ya kikazi mkoani Pwani na kutembelea wawekezaji wa Sapphire Float Glass watakaohusika na utengenezaji wa vioo huku uzalishaji ukitarajiwa kuanza mwezi Septemba, 2023.
Uwekezaji huu unatarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja zaidi ya 1650.
Aidha, Waziri Mkumbo amesisitiza nia ya serikali kuendelea kujenga mazingira bora na rahisi ya uwekezaji nchini ili kuvutia wawekezaji zaidi wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kujitosheleza kwa bidhaa na kuongeza thamani ya didhaa zinazosafirishwa nje ya nchi na kujipatia fedha zaidi za kigeni.