The House of Favourite Newspapers

Waziri Mazrui Apongeza Jitihada Za Vodacom Kuleta Maendeleo Kwa Jamii Katika Hafla Ya Iftaar

0
Waziri waAfya wa Zanzibar, MheshimiwaNassor Mazrui akizungumza kwenye iftar hiyo.

Waziri waAfya wa Zanzibar,Mheshimiwa Nassor Mazrui ameipongeza kampuni ya teknolojia na mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC kwa kushirikiana na serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuleta maendeleo kwa jamii.

Waziri Mazrui alisema hayo jana wakati wa Iftar ya pamoja iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wateja na washirika wake visiwani Zanzibar.

“Niwapongeze Vodacom kwakuwa mdau wa maendeleo na kwa kipekee zaidi napenda kutambua mchango wao mkubwa katika kuimarisha afya ya mama na mtoto kupitia mchango wa vifaa tiba pamoja na mfumo wa m-mama ambao tunatekeleza kwa pamoja hapa visiwani,”alifafanua Mh Mazrui.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B, Mh. Hamida Mussa amesisitiza wajibu wa sekta binafsi katika kuwawezesha wateja na wananchi huku akiipongeza kampuni ya Vodacom kwa mchango wao katika masuala ya afya, elimu na biashara.

“Karibuni sana Vodacom, sisi kama viongozi wa serikali, tupo tayari kuendeleza ushirikiano nanyi katika kuleta maendeleo kwa jamii,” alisema Mh.Mussa huku akidadavua kwamba maendeleo hupatikana panapokuwa na ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi.

Kwa upande wake, Mkuuwa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani kutoka Vodacom, Bi.Brigita Stephen alielezea furaha ya timu yake baada ya kujumuika na wateja wao wa Visiwani Zanzibar akitilia mkazo maono ya kampuni hiyo ya kutumia teknolojia ili kuboresha maisha ya Watanzania.

“Tumefurahi kujumuika na wateja pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Afya na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B katika hafla ya Iftar. Tumepata wasaa wa kujadili namna ya kukuza upatikanaji wa huduma na kuboresha ushirikiano na serikali yetu, na tuna ahidi kuendelea kuwa mdau namba moja wa maendeleo ya jamii yetu,” alisisitiza Bi. Stephen.

Leave A Reply