The House of Favourite Newspapers

Waziri Mgumba Alivyokagua Zao la Alizeti Singida

0
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe, Omary Mgumba amefanya  ziara ya siku Tatu mkoani Singida kwa ajili ya kukagua na kuhamisisha uzalishaji zaidi wa zao la Alizeti mkoani humo, kukagua shughuli za kilimo cha umwagiliaji pamoja na vyama vya ushirika.
Msingi wa ziara hiyo ni mkakati wa serikali katika juhudi za kuongeza uzalishiji wa zao hilo la alizeti ili kutatua changamoto ya upungufu wa malighafi kwa viwanda vya ndani vya kusindika mafuta ya kula kutokana na uzalishaji mdogo wa mbegu na kuilazimu serikali kutumia kiasi kikubwa cha pesa za kigeni kuagiza maguta ya kula nje ya nchi.
Katika ziara hiyo Mhe Mgumba alipata fursa pia ya kutembelea wadau wa zao la alizeti katika maeneo yao kwenye mnyororo wa thamani kuanzia mashambani kwa wakulima, wasindikahi wa viwanda vidogo, wa kati na wakubwa kama inavyoonekana kwenye picha mbalimbali. Pia alipata fursa ya  kutembelea ofisi za chama cha Mapinduzi wilaya na mkoa wa Singida.
Katika ziara hiyo ya siku tatu alitembelea wilaya za Singida, Manyoni na Mkarama. Pia alitembelea mashamba ya mikorosho mipya Wilayani manyoni.
Mgumba alipokea Changamoto za wadau kwa ajili ya kuzipatia majawabu na kuwaeleza mipango mbalimbali ya serikali katika kuinua tija na uzalishaji na uwekezaji katika kilimo cha alizeti ili kuondoa tatizo la upungufu wa mafuta ya kula ili kutengeza ajira, kukuza uchumi wa watu na taifa kwa ujumla.
Mikakakti hiyo ni pamoja na kuendelea na ujenzi wa vituo vya rasilimali kilimo kwenye kata ili kutoa taarifa, mbinu, teknolojia, haki ya hewa na masoko ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa wakulima ili kuwapatia huduma za ugani wakulima wengi na kwa wakati katika ngazi za chini.
Kuendelea kuajiri maafsa ugani  ili kutoa elimu kwa wakulima ili kuongeza tija na uzalishaji, kuwapatia mikopo wakulima kupitia  benki ya kilimo na benki washirika, mfuko wa pembejeo, kutengeneza mazingira mazuri ya kibiashara ili sekta binafsi kutoa mikopo ya mbegu bora za kisasa zenye mafuta mengi kwa mkopo kwa wakulima na kulipa baada ya mavuno kupitia kilimo cha mkataba, kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji vijijini ili kuongeza thamani ya alizeti kwa viwanda vidogo hukohuko vijijini na kuwauzia wenye viwanda hikubwa.
Mhe Mgumba pia alisema serikali kupitia wizara ya kilimo na wizara zingine za kisekta pamoja na wizara ya elimu zinaendelea na majadiliano ya kufungamanisha Elimu yetu ma kilimo chetu ili kuzalisha wataalaamu wakilimo wanaokidhi mahitaji ya soko la ajira kukuza kilimo chetu cha tija.
Mhe mgumba amemaliza ziara ya siku sita ya mikoa ya Manyara na Singida juzi na kuanza ziara ya siku tatu mkoani Dodoma.
Leave A Reply