The House of Favourite Newspapers

Waziri Mgumba awakumbusha wananchi faida za michezo

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mh. Omary Mgumba akifanya mazoezi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Omary Mgumba, amewataka watu wa rika mbalimbali kuwa na kawaida ya kushiriki katika michezo ikiwemo kufanya mazoezi.

Naibu Waziri huyo amezitaja faida za kufanya mazoezi na kushiriki michezo kuwa ni kulinda afya zetu na kutunza miili yetu.

“Tusitafute sababu na visingizio kwa kutofanya mazoezi, umuhimu wa mazoezi ni mkubwa sana.

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mh. Omary Mgumba akifanya mazoezi.

 

“Rai yangu kwenu tufanye mazoezi angalau saa mbili kwa siku kwa kuzingatia umri na ushauri wa madaktari wetu. Fanya mazoezi kwa mazingira ya ulipo, usisubiri mpaka uende uwanjani,” alisema.

 

Kiongozi huyo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amekuwa bega kwa bega katika kuhakikisha sekta yake ya kilimo inakuwa imara.

 

Licha ya muda mwingi kuwa kwenye kazi zake, lakini huwa anapata muda wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya yake.

Comments are closed.