The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkenda na Waziri wa Elimu Zanzibar Wapokea Taarifa ya Awali ya Sera ya Elimu

0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda akizungumza jambo katika kikao hicho.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Mohamed Leo tarehe 12 Septemba 2022 wameshiriki kikao kazi cha kamati ya mapitio ya sera ya elimu.
Katika kikao kazi hicho, Mawaziri hao wamepokea taarifa ya awali ya maendeleo ya kazi ya uchambuzi wa sera ya elimu.
Timu hiyo inayofanya kazi Jijini Dar es salam inaendelea na uchambuzi wa Sera ya Elimu ya mwaka 2014 ambapo Sera hiyo ilifuta sera ya elimu ya mwaka 1995.
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inapitia sera hiyo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati akihutubia bunge tarehe 22 Aprili mwaka huu jijini Dodoma.
Leave A Reply