The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Waziri Mkuu abaini upotevu wa makontena mengine 2,431

BREAKINGNEWS31Waziri Mkuu, Kassim M. Majaliwa.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim M. Majaliwa leo amefanya tena ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam na Shirika la Reli Tanzania (TRL) na kubaini upotevu wa makontena zaidi ya 2,431. Akiwa bandarini amekagua mfumo wa utoaji na uingizaji mizigo bandarini.

Katika maongezi ya awali Meneja wa Bandari alimuhakikishia kuwa mfumo hauruhusu kontena kuibiwa lakini Waziri Mkuu alienda na ripoti ya ukaguzi na kumuonyesha majina ya waliopitisha makontena zaidi 2,431 bila kulipiwa kodi.
Amempa muda wa masaa matatu hadi saa kumi na mbili jioni aambiwe hatua zilizochukuliwa kwa wahusika kwa sababu anawafahamu.
Katika hatua nyingine, Waziri mkuu alitembelea shirika la reli na kukuta mabilioni yametumika na miradi iliyokusudiwa haijatekelezwa.

Comments are closed.