Waziri Mkuu Aeleza Bil 3.5 Kujenga Km 4 za Sehemu ya Barabara ya Lami Jimbo la Mchinga Uanze Haraka
Waziri Mkuu wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa amemtaka meneja wa Tanroad Mkoa wa Lindi engener Emily Zengo kuanza haraka ujenzi wa barabara ya Milola kwa kiwango Cha Lami yenye urefu wa kilometa 4 .
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo akiwa kijijini hapo na kuwaahidi wanainchi waliojitokeza kurudi tena kijijini hapo kati ya tarehe 20 au tarehe 21/11/2024 Ili kujihajikishia jukumu aliloliagiza kuwa limetekelezwa.Mradi huo wa barabara kwa kiwango Cha Lami utagharimupesa ya Kitanzania Shilingi bilioni3.5
“Mhandisi nataka nijue mkandarasi ataanza kazi lini meneja wa Tanroad hii Mimi ndiyo barabara yangu ee nikitoka huko Mimi nitapita hapa kwenda kijijini tutakua tumesha maliza bunge na tutakuja huku na muheshimiwa mbunge tutakuja kuona kama umeanza kazi.; Amesema Waziri Mkuu
Aidha Muhandisi Zengo amemuahidi waziri Mkuu kuanza haraka kwa ujenzi huo na jumaatatu 21/10/2024 wataalamu ambao wataanza na kazi ya kusanifu wa kazi ambayo inaweza kuchukua siku 14 na baada ya hapo utaanza mchakato wa kumtafuta mkandarasi.
Muhandisi Zengo pia Amesema baada ya wataalamu kusanifu sehemu hiyo ya barabara mkandarasi ataanza kazi rasmi tarehe 18/11/2024 ikiwa ni mwezi mmoja baada ya agizo kutolewa.
Naye Salama Kikwete mbunge wa jimbo alisema anamshukuru serikali ya mama Samia kwakulifa Jimbo la mchinga kua namabadiliko katka maeneo yote muhimu japo Kuna changamoto ya Madaraja mengi kutokana na mvua kubwa zilizo nyesha mwaka huu na kusababisha uharibifu Mkubwa wa muundo mbinu.
Pia Mama Salama Kikwete Amesema japokua kila eneo limekua na mabadiliko makubwa kwasasa wanahitaji Kituo Cha Afya Milola ambacho tayari Kiko kwenye Mpango wa kuanza ujenzi na kilio kingine ni Lami Ili kuunganisha Ruangwa na Milola kuelekea Ngongo.
“Mh Waziri Mkuu kilio Cha wanainchi wa jimbo la mchinga kilio kikubwa ni suala Lami kuanzia Milola Hadi Ngongo wanainchi Hawa wanatamani sana Lami na ukisha leta Lami wanainchi hawatakua na neno la kusema kwasababu kila kitu kitakua kimekaa sawa”
Aisha Selemani mwanainchi Amesema anamshukuru serikali ya awamu ya Sita pamoja na mbunge wao kwa kuwaletea mabadiliko makubwa jimboni kwao na hawana mashaka tena .
“Tunamshukuru Rais Samia na Mama Salma kwakuendelea kutuletea maendeleo jimboni kwetu watoto wanasoma kwa Amani maji yanapatikana umeme unawaka na Leo tume msikia waziri Mkuu ametoa agizo la kuja kuwekwa Lami hapa tutakua tumemaliza”Amesema Aisha
Nae Mudhiri Majangwa Amesema amefurahishwa na kitendo Cha waziri Mkuu kutoa maelekezo ya kuanza kwa haraka ujenzi wa sehemu ya kilo mita 4 Za barabara Katika Kijiji hicho na kwa kufanya hivyo baada ya kukamilika ujenzi huo anaamini Milola itakua na mabadiliko makubwa.
“Nimefurahi kusikia waziri Mkuu anatoa maagizo ya ujenzi wa barabara kwa meneja kwetu sisi Wana Milola ni furaha na faraja kubwa mji wetu utabadilika tufanya biashara Hadi usiku kwasababu baada ya barabara kukamilika tutaka chini ya taa zitakazo na wekwa biashara zetu”