The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Afungua Kongamano la Bakwata Kuhusu Madawa

0

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amefungua rasmi kongamano Maalum la Kujadili Mmomonyoko wa Maadili na Athari za Dawa za kulevya kwa vijana Dar es Salaam.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Alhad Mussa Salum, akizungumza jambo wakati wa konamano hilo.

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) chini ya Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh, Abubakar Zuberi, limehudhuriwa na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa dini za Kiislam, Kikristo wasiokuwa waumini.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers William Sianga, akifafanua jambo.

Mbali na viopngozi wa dini, kongamano hilo limehudhuriwa na viongozi wa serikali wakiwemo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers William Sianga, Naibu Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jaffo na wengine.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akizindua kongamano hilo.

Azkizungumza wakati wa uzinduzi wa kongamano hilo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewashukuru viongozi wa dini kwa kuwa msitari wa mbele kuwahutubia waumini wao kwenye nyumba za ibada wakiwahamasisha kuachana na matumizi ya dawa za kulevya ili warudie hali zao za kawaida na kuendeleza ujenzi wa Taifa..

Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakary Zubeiry bin Ally, akizungumza wakati wa kongamano hilo.

Majaliwa amesema, “Ninaamini kuwa, kongamano hili litakuiwa na manufaa makubwa kwani litaweza kuhimiza vijana kuwa na maadili mema, athari za kutumia madawa na kuwajengea mazoea ya kutenda mambo yaliyo mema ili wasije wakajiingiza katika matatizo yanayoweza kuhatarisha maisha yao.”

Majaliwa akizungumza.

Aidha Majaliwa ameeleza mbinu nyingine ambayo watumiaji wa madawa ya kulevya wamekuwa wakitumia gundi ya maji ‘patex’  kuvuta. Akizungumzia suala hilo, Majaliwa amesema kuwa, Serikali inaadaa mkakati wa kupiga marufuku uingizwaji wa gundi hiyo ambayo hutumika katika kuziba pacha na kugundishia viatu pamoja na kuondoa viashiria vingine vya madawa ya kulevya nchini..

Kongamano likiendelea. 

Naibu Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jaffo

Baadhi ya watu waliohudhuria kongamano hilo.

NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply